Jumatano , 23rd Oct , 2019

Rais Magufuli amemteua Mh. Cleopa David Msuya (Waziri Mkuu Mstaafu) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) kwa kipindi kingine cha miaka miwili.

Rais Magufuli na Cleopa David Msuya

Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Oktoba 23, 2019, imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza jana Oktoba 22, 2019.

Msuya amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili tofauti akianza Novemba 7, 1980 hadi Februari 24, 1983 kisha kuongoza tena Desemba 7, 1994 hadi Novemba 28, 1995.