Jumamosi , 15th Oct , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Octoba 15, 2022 ametembelea na kuomba dua kwenye kaburi la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kumsalimia Mama mzazi wa Hayati Dk. Magufuli Bibi Suzana Magufuli.

Awali Rais Samia alitembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Wilaya ya Chato mkoani Geita akiwa katika ziara mkoani amesema serikali itahakikisha hospitali hiyo inakamilika na kuongeza wataalamu katika hospitali hiyo.

“Niwahahakishie kwamba Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato sasa majengo matano yapo tayari lakini hospitali haijaisha, niwahakikishie tutaijenga kama tulivyokusudia, wataalamu wa kutosha tumeshaleta na tutaendedelea kuleta” - Rais Samia

Aidha Rais Samia amewaomba wananchi kulipia bima za afya kwani kupitia bima hizo serikali itaboresha zaidi huduma za afya.

"Niwaombe sana tutakapokuja na mfumo wa bima ya afya kwa wote, wote tukalipie bima na kupitia bima hizo tunaweza kuboresha zaidi na zaidi huduma hizi za afya" – Rais Samia