Kujinyonga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, amesema Jeshi la Polisi mkoani humo, linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na kutangaza doria maalum ya kuwasaka watu ambao inadaiwa wana nia ya kutaka kujinyonga.
"Kwa vile sisi ni wataalamu, tutaanza kufanya doria kwa wote ambao wanatarajia kujinyonga, tutawakamata kabla hawajajinyonga na tutawapeleka mahakamani" amesema RPC Mwakalukwa.
#HABARI Watu wawili mkoani Tabora wamekutwa wakiwa wamejinyonga ndani ya nyumba zao walizokuwa wakiishi, huku chanzo cha tukio moja kikielezwa kuwa ni migogoro ya kifamilia.
RPC Tabora Mwakalukwa amesema wanafanya uchunguzi wa matukio hayo. pic.twitter.com/ckQ5gcmqfT
— East Africa TV (@eastafricatv) January 3, 2020
Tazama video kamili hapo chini.

