Jumatano , 21st Mei , 2014

Wakala wa Vipimo nchini Tanzania (WMA), umesema upo kwenye mchakato wa kuandaa Kanuni za upimaji na vipimo vya gesi asilia.

Mfanyabiashara akipima uzito na ujazo katika moja ya mitungi ya gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya vipimo duniani, Kaimu Meneja wa Habari wa WMA Irene John amesema kuwa kanuni hiyo imepelekwa kwa Waziri husika na inatarajiwa kuingizwa kwenye bajeti ya fedha ya 2014/ 2015.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upimaji, Ugezi na Huduma za Ufungashaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Agnes Mneney amesema kuwa ili kusaidia maendeleo ya viwanda na biashara ni lazima vipimo vifanane duniani kote na viweze kuthibitishwa kuwa vina uhakika, ni bora na vya kuaminika.