
Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda, wakati akifungua warsha ya siku mbili ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza umaskini awamu ya tatu katika mkoa wa Arusha, ambapo warsha hiyo imelenga kutoa taarifa, kuelimisha taratibu za kupunguza umaskini katika mkoa wa Arusha .
Amesema katika mkoa wa Arusha mradi huo unatekelezwa katika wilaya za Ngorongoro,Monduli,Longido ,Arusha,Meru ,Karatu na halmashauri ya jiji la Arusha.
Aidha kwa upande wa Mkoa wa Njombe halmashauri za wilaya zitakazohusika ni pamoja na Ludewa ,Makete,Njombe,Wanging’ombe na halmashauri ya miji ya Mkambako na Njombe.
Ameongeza kuwa awamu ya Tatu,tasaf ilizunduliwa na rais Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma ,ambapo alieleza undani wa umuhimu wa kutia mkazo katika suala la utekelezaji wa miradi ya huduma za elimu afya na maji na kuondoa umaskini wa kipato.
Amesema utekelezaji wa mradi wa awamu ya tatu ya tasaf umelenga sehemu nne ambazo ni kutoa ruzuku kwa kaya maskini ili ziweze kupata huduma za elimu na afya,kutoa ajira za muda kwa kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi .
Ntibenda amesema serikali imejiandaa vya kutosha kuhakikisha miradi ya kupunguza umaskini awanu ya tatu, katika halmashauri zote hapa nchini unatekelezwa ka asilimia 100.
Awali mkurugenzi wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo, umefanikiwa kuandikisha na kuvitambua vijijini kwa asilimia 70 katika halmashauri zote 159 hapa nchini zikiwemo Pemba na Unguja ili ziweze kunufaika na mradi wa kulipwa fedha na kupatiwa ajira za muda.
Amesema Tasaf awamu ya tatu,imepata ufadhili wa fedha kutoka chama cha waarabu wanaozalisha mafuta (OPEC)kiasai cha shilingi milioni 16.4 zitakazotekelezwa katika mikoa miwili ya Arusha na Njombe zitakazotumika kupunguza umaskini katika mikoa hiyo.