Jumatatu , 27th Jun , 2016

Vijana Mkoani Mtwara, wameshauriwa kuunda vikundi vya ujasiriamali, vitakavyowawezesha kupata mikopo kwa urahisi na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayowakwamua kiuchumi.

Vijana wakiwa katika mafunzo ya Ujasirimali(Picha na Maktaba).

Wakizungumza katika baraza la vijana lililofanyika mkoani humo vijana hao wamesema vikundi vya pamoja vitawawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha na mashirika mbalimbali kupitia umoja wao.

Vijana hao ambao wamepata mafunzo mbalimbali kupitia mradi wa Youth Economic Empowerment, ambao unawawezesha vijana kiuchumi wamesema kwa sasa wanatambua fursa walizonazo katika kuchochea maendeleo yao kwa kuanzisha vikundi vitakavyowasaidia kuongezea kipato.

Kwa upande wake Afisa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika la CODET, Royo Masanja amesema wamefanikiwa kuwahamasisha vijana kuunda vikundi na kuwapatia elimu ya utunzaji wa akiba.