'Viongozi wananiuliza kama mzee analala' - Makonda

Jumanne , 11th Feb , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Mgufuli kwa utendaji wake wa kazi na kwamba imefikia hatua hadi viongozi wa dini wanamuuliza kama Rais huwa analala kweli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Makonda ameyabainisha hayo leo Februari 11,2020, wakati wa uzinduzi wa Wilaya ya Kigamboni kwa kuzindua ofisi ya Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya na Jengo la Utawala pamoja na Hospitali kubwa ya Wilaya.

'Viongozi wa dini kila siku wananiambia hivi mzee analala kweli, nawaambia analala kwa maombi yenu, unawaza Watanzania kuliko hata familia yako, unatufundisha ambayo hatukuwahi kujifunza, zamani tulikuwa tunanyosha mti kumbe kimvuli kimepinda, Mh Rais hata sisi vimvuli tumenyooka' amesema Makonda.

Aidha Makonda amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha siku ya Februari 14, wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la uhuishaji wa taarifa zao katika daftari la mpiga kura