Ijumaa , 14th Aug , 2015

Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Dar es Selaam, Lindi, Mtwara na Ruvuma wanapatiwa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.

Mkufunzi kutoka Shirika la BBC Media Action, Ichikaeli Maro.

Akizungumza mara baada ya kufungua mafunzo hayo leo Mkoani Mtwara, Mkufunzi kutoka Shirika la BBC Media Action, Ichikaeli Maro, amesema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa tofauti na chaguzi zingine zilizopita kutokana na kuwa na wagombea wengi na vyama vingi vya siasa huku muamko wa kisiasa kwa wananchi ukiwa juu.

Kwa upande wake, katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Selaam, Hussen Mgongolwa, amesema wapo baadhi ya waandishi ambao wanakumbwa na changamoto kutokana na kufanya kazi katika vyombo ambavyo wamiliki wake wanaushabiki na baadhi ya wanasiasa na kupelekea kuwaingiza katika matatizo

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa siku tatu na Shirika la BBC Media Action kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwa lengo la kuwafanya waandishi wahepukane na kuwa sehemu ya chanzo cha migogoro au vurugu zinazotokana na uchaguzi.