
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge kilimo, Mifugo na maji
Kauli hiyo wameitoa mara baada ya kukagua chanzo hicho cha maji kilichopo Butimba wilayani Nyamagana jijini Mwanza kilichogharimu shilingi bilioni 69 ambapo kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 48 kwa siku.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Almas Maige amesema hawataweza kuwavumilia wakandarasi wazembe kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Maryprisca Mahundi ambaye ni Naibu Waziri wa Maji akaahidi kusimamia kikamilifu ujenzi wa chanzo hicho cha maji ili uweze kukamilika kwa wakati na wakazi wa jiji la Mwanza wapate maji.