
Miili hiyo iligundulika ijumaa iliyopita mingi ikiwa imeunguzwa ndani ya boti waliyokuwemo.
Umoja wa mataifa nchini Libya umesema kuwa mauaji hayo yamesababishwa na ugomvi baina ya magenge ya biashara ya kusafirisha watu na kutaka wahusika wote kufukishwa mbele ya mkono wa sheria.
Libya imekua ni kitovu kikuu cha magendo ya kuwasafirisha wahamiaji haramu kuelekea Ulaya.