Jumapili , 20th Nov , 2016

Kiongozi wa chama cha waandishi wa habari nchini Misri, na wakuu wengine wawili, wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili, kwa kuwapa hifadhi wenzao waliokuwa wakisakwa na polisi.

Yahia Kallash, kiongozi wa chama cha waandishi wa habari nchini Misri

 

Hukumu hiyo, ambayo inaweza kufutwa wakilipa faini ya dola mia sita, imetokana na msako wa polisi kwenye ofisi ya jumuiya ya wafanyakazi mjini Cairo mwezi wa Mei, wakati polisi wa nchi hiyo walipokuwa wakiwasaka waandishi wa habari wawili.

Wanahabari waliokamatwa walishutumiwa kulalamika juu ya uamuzi wa serikali ya Misri, kuikabidhi Saudi Arabia, visiwa viwili katika Bahari ya Sham.