Walichokisema Madiwani 8 wa CUF waliohamia CCM

Alhamisi , 16th Jan , 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amewapokea Madiwani nane waliokuwa wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally akihutuia mkutano wa hadhara Tanga

Madiwani hao waliohamia CUF, wameongozwa na Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Tanga Bashiru Azizi na Naibu Meya wa jiji la Tanga Haniu Ally huku Madiwani wengine  ni Mswahili Njama (Chongoleani), Said Alei (Masiwani) na Habibu Mpa (Ngamiani).

Nassoro Salimu Diwani (Tongoni), Akida O. Akida (Ngamiani Kaskazini), Mwanaisha Abdala Diwani Viti Maalum, Thurekha Mahadhi Diwani Viti Maalum Ngamiani na Mke wa Mbunge wa CUF wa Tanga Mjini.

Madiwani hao waliojiunga na CCM wameeleza sababu kukihama chama hiko, ikiwa ni pamoja na vyama vyao kukosa dira ya uongozi na kuelekea kupoteza uhalali wa kuomba ridhaa ya kuwaongoza Watanzania.