
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda
Waziri Mkenda ametoa maagizo hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Walimu duniani iliyofanyika wilayani Bukombe Mkoani Geita huku akiwasisitiza Walimu kutoa taarifa juu ya maeneo yenye ili serikali iweze kuyafikia.
"Naona kuna clip inazunguka mtandaoni, wanafunzi wamelala wanaandika wengine mtakuwa mmeiona Sasa nimetumiwa na watu wengi sana, kwahiyo sisi tungependa pence changamoto tuambizane, pahali popote pence changamoto walimu wangu tushirikiane wadhibiti ubora wakurugenzi wa halmashauri tumalize changamoto, shule ambazo zina changamoto ya Vyoo, Mabweni, Vitanda na kila kitu twendeni, siamini hizi changamoto zikija na madiwani wako pale kwamba tutashindwa kutatua kwa nchi nzima kwahiyo tupeane taarifa tufanye kazi na wadhibiti ubora niliwaambia ni mboni ya jicho letu", alisema Mkenda
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Bukombe Dokta Dotto Biteko anasema serikali kwa kutambua changamoto ya miundombinu wilayani humo imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
"Na nichukue nafasi hii kumshukuru mheshimiwa Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwanza kwa kuiangalia Bukombe kwa jicho la kipekee na kuendelea kuiletea mabilioni ya fedha kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kwenye sekta ya Elimu, madarasa ambayo tulikuwa tukizungumza kwa muda mrefu mama ameendelea kuleta fedha na mwaka huu kama alivyosema mheshimiwa mkuu wa wilaya tutajenga madarasa mengine zaidi ya 170 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mazingira mnayofanyia kazi yanakuwa bora zaidi", alisema Biteko.
Baadhi ya walimu walioshiriki maadhimisho haya wameishukuru serikali kwa kuandaa siku maalum kwa ajili ya kuwaenzi walimu huku wakielezea changamoto zilizopo shuleni mwao.
"Madawati ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wetu wa shule za msingi wengi wanakaa wanne wanne watano watano kwenye dawati moja kitu ambacho kimawatia ugumu katika ujifunzaji, nawahamasisha wazazi ma serikali waungane kitu kimoja ili kutatua changamoto ya madawati ya wanafunzi", alisema Kaswahili.
"Nashauri wadau mbalimbali watusaidie, serikali inafanya jambo kubwa sana huwa kila mwezi wanaleta Pad shuleni kwa ajili ya wanafunzi wa kike pia tunashauri wadau wengine mbalimbali wawe wanasaidia shule za shule za sekondari shule za msingi kutuletea taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wetu kujistiri na kupata Elimu bora", alisema Mwagisa.