Jumanne , 26th Jul , 2022

Wananchi wa kijiji na kata ya Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wamelazimika kufunga barabara na kuzuia msafara wa Waziri wa maji, wakishinikiza Serikali kutoa ufafanuzi kwa kata hiyo kukosa huduma ya maji safi na salama

Mmoja wa wananchi amesema licha ya kuwepo mradi unaojengwa kijijini hapo, mradi umechukua mda mrefu na kusababisha wananchi kuendelee kukosa maji na kutumia ya visima na mito yasiyo salama.

Akitolea ufafanuzi wa mradi unaotekelezwa kutokamilika kwa wakati, Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA mhandisi Mathiaus Mwenda amesema mradi umefikia asilimia 90

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Uvinza Hanafi Msabaha amekiri kata hiyo kutokuwa na huduma ya maji, na kwamba mradi unaotekelezwa licha ya kutumia gharama kubwa bado umekuwa na kusua sua kukamilika

Waziri wa maji Jumaa Aweso ametoa maelekezo kwa RUWASA na kutaka ndani ya wiki moja vifaa viwe vimefika na mradi uanze kazi mara moja ya kuhudumia wananchi.