Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Maafisa na Watendaji mbalimbali wa Utumishi wametakiwa kuwawekea mazingira mazuri watumishi wengie wa Umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu na kwa wakati.

Waziri wa nchi Ofisi ya rais na Utawala Bora. Mhe Angela Kairuki,

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma, Jijini Arusha, Waziri wa nchi Ofisi ya rais na Utawala Bora. Mhe Angela Kairuki, amesema kuwa watumishi wa Umma wanatumia muda mwingi kuwahudumia wananchi hivyo ni lazima wawe na mazingira mazuri ya ufanyaji kazi.

Mhe. Kairuki amesema kuwa Maafisa na Watendaji mbalimbali waliopewa dhamana hawatekelezi dhamani ya nafasi zao kama walivyokusudia huku wengine wakiwajali zaidi wateja wao wa nje kuliko wateja wa ndani ambao ni watumishi wa umma.

Aidha Waziri huyo amewataka watumishi wa Umma kutokuogopa kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo wanapoona kuwa hawatendewi haki katika maeneo yao ya kazi ili hatua za haraka zichukuliwe.

June ya Wiki ya Utumishi wa Umma, imeanza kuadhimishwa kuanzia June 16 ambapo kilele chake ni leo June 23.

Waziri wa nchi Ofisi ya rais na Utawala Bora. Mhe Angela Kairuki,