Jumamosi , 19th Jan , 2019

Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Anitha, ameweka wazi sababu za kuwachanganya kimapenzi wasanii wawili, mpaka kufikia hatua ya kuitwa 'Chawote na mmoja ya wasanii hao.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Televisio, Anitha amesema kwamba alikuwa kwenye mahusiano na Gig Cartel lakini alidumu naye kwa miezi sita tu, kwani hawezi kukaa na mwanaume kwa muda mrefu kiasi hicho.

“Gib Carter nilikuwa naye kwa miezi sita, huwezi ukakaa na mwanaume kwa muda wote huo, si unachoka, sio kwamba siwezi kudumu, ila unajua kuna vitu vinakuwa vinakosekana, unajua mtu akishaingia kwenye mahusiano anajisahau, na mwanamke anahitaji matunzo”, amesema Anitha.

Kutokana na hiyo ndio sababu iliyomfanya akaamua kuwa na mahusiano na msanii Bright, na ndio kilichopelekea kupewa jina la 'Chawote' na Bright, kitendo ambacho anadai ni kumdhalilisha huku akimtaka amuombe msamaha.