Jumamosi , 18th Jan , 2020

Kupitia kipindi cha Friday Night Live "FNL" ya East Africa Tv kinachoruka kila siku ya ijumaa kuanzia 9:00 kamili usiku, msanii Aslay  amefunguka uwezekano wa kurudiana mzazi mwenzie aitwaye Tessy Chocolate, pamoja na malezi ya mtoto wao.

Pichani ni msanii Aslay na mzazi mwenziye Tessy Chocolate

Akizungumzia uwezekano wa  kurudiana na mama wa mtoto wake huyo Aslay amesema kuwa, 
"Hakuna kitu kama hicho na haiwezekani, kila mtu ameshaondoka kivyake na kuangalia maisha yake, kikubwa ni mtoto wetu akue tumuombe maisha mema kilichobaki ni kuheshimiana tu sasa hivi, Mimi mwanangu muda ambao hayuko shule huwaga nipo naye sana" ameeleza

Aidha Aslay ameendelea kusema "Mwanangu akiniambia akitaka kuimba ni sawa tu, mtu afanye kile anachokiona kiko sawa kikubwa kisimuharibie kwenye maisha, pia mwanangu yupo kwenye video yangu ya moyo kiburi" ameongeza

Msanii huyo ameachia Extended Player ambayo ina nyimbo 9, ila mwenyewe amesema kati ya nyimbo zote hizo anazozikubali na anazozitegemea ni tatu tu.