Jumamosi , 3rd Sep , 2016

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema limeridhishwa na kiwango cha washiriki wa Dance100% ambacho kimeoneshwa leo wakati wa hatua ya nusu fainali katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam.

Makundi matano yaliyoingia fainali mara baada ya kutangazwa

Akizungumza na EATV Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bwn. Kurwijira N Maregesi amesema makundi mengi yameonesha kiwango cha kuridhisha na kuonesha kwamba walijipanga katika kuhakikisha kwamba wanajinyakulia ushindi wa shindano la Dance100%.

“Ukweli nimefurahishwa na kiwango cha washiriki, ambapo kuna makundi ambayo yalijiandaa kwa kumaanisha na matokeo yake tumeyaona walivyokuwa jukwaani, na ambao walijiandaa kwa kusuasua matokeo yake pia hayajajificha , imeonekana wazi walijiandaa kwa kujaribu, hivyo tunawapongeza ambao wanazidi kuchukulia mashindano haya kama fursa kubwa ya wao kutoka kimaisha” Amesema Maregesi.

Maregesi ameongeza kuwa shindano la Dance100% limesaidia kufanya vijana kuwa pamoja na kufanya mazoezi jambo ambalo linawafanya kujenga udugu pamoja na kujenga afya, vilevile kuweza kushirikiana katika mambo mbalimbali yenye tija katika jamii, hivyo waandaaji tunawapongeza sana kwani imedhihirika mchango wao ni wenye tija kwa jamii.

Shindano la Dance100% linaendeshwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom na Coca Cola na kuoneshwa siku yan Jumapili saa moja jioni EATV pekee.

Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bwn. Kurwijira N Maregesi
Tags: