Alhamisi , 19th Mei , 2022

Huenda ungemsikia Jux kwenye ngoma ya Naogopa ambayo amefanya Marioo na Harmonize kama mambo yasingekuwa mengi au ratiba zake kuingiliana.

Kulia ni msanii Juma Jux kushoto ni Producer Abbah

Taarifa hiyo ameitoa Abbah Process, producer wa ngoma hiyo ya naogopa wakati anapiga story na Big Chawa kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

"Hii beat ya Naogopa mara ya kwanza nilifanya na Jux, baada ya kuitengeneza Jux alikuwa hana 'Mood' kwa sababu alikuwa amechoka, kila tukipanga tufanye kinatokea hichi mara kile labda 'Feeling' zake hazikuwa zime-click kwenye huu mziki pengine" amesema Producer Abbah Process