Jumanne , 22nd Jun , 2021

Nyota wa muziki wa RnB Chris Brown ameripotiwa kuchunguzwa baada ya mwanamke mmoja kudai kumshambuliwa nyumbani kwake  huko Los Angeles mwishoni mwa wiki. 

Picha ya msanii Chris Brown

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa zinadai kuwa ulitokea mzozo kati ya Breezy na mwanamke huyo ambaye jina lake halijawekwa wazi ndipo akampiga kofi kali mpaka kusababisha weave yake kutoka inagwa hakupata majeraha kando ya weave anayedaiwa kutolewa.

Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa lakini mamlaka ilithibitisha kwamba polisi walifika nyumbani kwake kufuatia tukio hilo linalodaiwa baada ya kutajwa kama mtuhumiwa katika ripoti ya polisi.