Jumanne , 1st Jun , 2021

CEO wa lebo ya High Table Sound na msanii Barnaba Classic amewatoa hofu wapenzi wa muziki kwa madai ya wimbo wake mpya wa cheketua kufanana na wimbo wa dodo ya Alikiba alioutoa mwaka jana 2020.

Picha ya msanii Barnaba

Barnaba Classic amesema aliupenda wimbo wa dodo ndio maana kuna baadhi ya vionjo vya wimbo huo kwenye kazi yake mpya ila cha msingi watu wa-enjoy muziki mzuri na mirindimo hiyo isiwachanganye.

"Mirindimo ya Cheketua wanasema imefanana na Dodo ya Alikiba lakini tulicho-deliver ni kitu kizuri na watu wanapenda, sawa na sukari inabadilika tu majina lakini utamu ni ule ule, kwa hiyo mirindimo ya ngoma isiwachanganye" ameeleza Barnaba