Jumatatu , 23rd Mar , 2015

Daddy Face amesema kuwa wimbo wake wa Forever ni maalum kwa kuonesha upendo kwa mpenzi wako, anaamini kwamba kila mtu anapokuwa katika mahusiano lazima umpende mpenzi wako forever na umuoneshe kwa vitendo kwamba kweli utakuwa naye forever

Daddy Face amesema kuwa wimbo wake wa Forever ni maalum kwa kuonesha upendo kwa mpenzi wako, anaamini kwamba kila mtu anapokuwa katika mahusiano lazima umpende mpenzi wako forever na umuoneshe kwa vitendo kwamba kweli utakuwa naye forever.

“Forever ni wimbo unaohusu mapenzi na kama ujuavyo hisia huwasilishwa kupitia nyimbo na ndio maana nikatunga wimbo huu. Ujumbe katika wimbo huu ni kuwakumbusha watu kuwapenda wapenzi wao forever, kuwathamini, kumjali na kumheshimu hii ndio ngao kubwa katika mapenzi. Amesema Daddy Face

Hadi sasa Daddy Face ameshatoa nyimbo karibia tano zikiwa na ujumbe tofauti, ingawa kwa sasa makazi yake ni Marekani ila Daddy Face mzaliwa wa Burundi na akakulia Tanzania hivyo amesema lengo langu kubwa ni kuwapa watu wa Afrika Mashariki nyimbo nzuri.

“ Napenda kuomba sapoti toka Watu wa Afrika Mashariki hapa naamanisha Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda maana lengo langu kubwa wao ni kuzifahamu nyimbo zangu na pia kuzipenda. Baada ya Forever napanga kuachia wimbo mwingine ila kwa sasa waweza tembelea you tube na ku-search jina la Daddy Face na utaona nyimbo zangu” Aliongeza Daddy Face

Hii ni kazi ya Daddy Face iitwayo Forever iliyoko you tube, waweza itazama pale kwa kubofya link hii https://www.youtube.com/watch?v=HgLGls184WE