Jumanne , 21st Dec , 2021

Mkali wa muziki wa singeli Dullah Makabila ameshea video kwenye page yake ya Instagram akikabidhiwa gari mpya aina ya Subaru Forester aliyonunuliwa na mke wake.

Msanii Dullah Makabila akiingia kwenye gari hiyo mpya

Dullah Makabila ameandika ujumbe huu wakati anapewa gari hilo.

"Mpaka muda huu bado siamini kama mke wangu ameamua kuninunulia zawadi ya gari ya kifahari kiukweli nimefurahi asante sana mke wangu, kwenye macho yao naweza kusimama kama mwanaum e asiye na maana mbele ya msichana mwenye mafanikio kama wewe".

"Nakuahidi nitaitunza gari hii moyoni mwangu kwanza kabla sijaipeleka gereji yeyote bora hapa mjini".