Jumanne , 25th Mar , 2014

Majina ya wasanii na makundi mbalimbali ya muziki yatakayowania tuzo mahiri za muziki za Kilimanjaro kwa mwaka 2014, yametangazwa leo jijini Dar es Salaam.

Katika vipengele mbalimbali vilivyotangazwa, mwanadada Lady Jay Dee ameweza kuongoza kwa kutokea katika vipengele 5 ambapo pia kwenye moja ya kipengele anatajwa kuwania tuzo hizo mara mbili.

Mwanadada huyu anafuatiwa kwa karibu na mwanamuziki Diamond Platinumz ambaye anawania tuzo hizo katika vipengele vitano, akifuatiwa na Ommy Dimpoz, Cassim na Ben Pol, G Nako Fid Q na msanii Young Killer ambao wote wanafungana kwa kutokea katika vipengele vitatu.

Majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo maarufu za muziki nchini Tanzania yametangazwa na Mratibu wa tuzo hizo kutoka BASATA Kurwijira Maregesi, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Nyimbo ya Uzuri Wako ya Jux, Tema Mate Tuwachape ya Madee na Nimevurugwa ya Snura, ni miongoni mwa nyimbo zilizoondolewa katika mchakato wa kushindania tuzo kwa sababu za kimaadili na maudhui.

Tuzo hizi zitatolewa rasmi tarehe 3 mwezi Mei mwaka huu zikitanguliwa na zoezi la kupigiwa kura kwa washiriki ili kupata washindi, zoezi ambalo litaanza rasmi tarehe 1 mpaka 31 mwezi April.

Unaweza kuona nominations zote hapa;

Kilimanjaro Lager ‏@Kili_Lager now

Mwimbaji Bora wa Kike - Bendi
Luiza Mbutu
Catherine Cindy
Ciana

Mtunzi Bora Taarab
Mzee Yusuf
El-Ahad Omary
El-Khatib Rajab
Kapten Temba
Sadiki Abdul
Nassoro Seif

Mwimbaji Bora Kiume - Bendi
Jose Mara
Kalala Junior
Charz Baba
Khalid Chokoraa
Christian Bella

Mwimbaji Bora Kiume - Taarab
Mzee Yusuf Hashimu
Saidi Mohamed
Ali aka Mtoto Pori

Mwimbaji Bora wa Kike - Taaarab
Khadija Kopa Isha Ramadhani
Khadija Yusuph
Mwanahawa Ali
Leyla Rashid

Kikundi cha Mwaka - Taarab
Jahazi Modern Taarab
Mashauzi Classic
Five Stars

Kikundi Cha Mwaka - Kizazi Kipya
Makomandoo
Navy Kenzo
Weusi
Mkubwa na Wanawe

Bendi ya Mwaka:
FM Academia
Mapacha Watatu
Twanga Pepeta
Akudo Impact
Malaika Band
Mashujaa Band

Mtunzi Bora wa Mwaka Band
Christian Bella
Jose Mara
Chaz Baba
Nyosh El Saadat
Kalala Junior

Video Bora ya Mwaka
Number One - Diamond
Yahaya - Lady Jaydee
Joto Hasira - Lady Jaydee
Uswazi Takeaway - Chege
Mama yeyo - GNako

Mtumbuizaji Bora wa Kiume Kizazi Kipya:
Diamond
Christian Bella
Rich Mavoko
Ommy Dimpoz
Abdul Kiba

Mtunzi Bora Hip Hop
Nikki wa Pili
Young Killer
ROMA
Fid Q
G-Nako

Mtunzi Bora wa Mwaka - Kizazi Kipya
Belle 9
Ben Pol
Diamond
Rama Dee
Rich Mavoko

Prodyuza Bora:
Marco Chali
Man Water
Mazoo
Sheddy Clever
Nahreel

Msanii Bora Chipukizi
Young Killer
Walter Chilambo
Y Tony
Snura
Meninah

Msanii Bora Hip Hop:
Fid Q
Stamina
Young Killer
Nick wa Pili
G-Nako

Mwimbaji Bora wa Kiume Kizazi Kipya:
Ben Pol
Rich Mavoko
Diamond Platnumz
Ommy Dimpoz
Cassim Mganga

Mwimbaji Bora wa Kike - Kizazi Kipya
Vanessa Mdee
Lady Jaydee
Linah
Maua Samma

Wimbo Zouk Rhumba
Yahaya - Lady Jaydee
Yamoto - Mkubwa na Wanawe
Msaliti - Christian Bella
Nakuhitaji - Malaika Band
Narudi kazini - Beka

Wimbo R&B
Listen - Belle 9
Closer - Vanessa Mdee
So Crazy - Maua Samma
Kama Huwezi - Rama Dee
Wa Ubani - Ben Pol

Wimbo Hip Hop
Bei ya Mkaa - Weusi
Nje ya Box - Nick wa Pili
Siri ya Mchezo - Fid Q
2030 - ROMA
Pesa - Mr Blue

Wimbo Afro Pop
Number One - Diamond
Joto Hasira - Lady Jaydee
Kidela - Abdul Kiba
I love u - Cassim
Tupogo - Ommy Dimpoz
Roho Yangu - Mavoko

Wimbo wa Band
Ushamba Mzigo - Mashujaa
Shamba la Bibi - Victoria sound
Chuki nini - FM Academia
Yarabi nafsi - Mapacha 3
Kiapo - Talent Band

Wimbo Bora wa mwaka: Number one - Diamond
Joto Hasira - Jaydee
I love u - Cassim
Yahaya - Lady Jaydee
Kidela - Abdul Kiba
Muziki Gani - Nay