Johari atangaza kufunga ndoa hivi karibuni

Alhamisi , 16th Jan , 2020

Msanii wa filamu Johari Chagula, amesema siku ya ndoa yake atatamani asherehekee na mashabiki zake kwa sababu wamechangia vitu vingi hadi kufika hapo alipo kwa sasa.

Msanii wa filamu Johari

Akipiga stori na Big Chawa kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni, Johari amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano rasmi na mtu ambaye ana malengo naye.

"Ni kweli nipo kwenye mahusinao, tuombe Mungu ikifika haina shida na kila kitu kitawekwa wazi, harusi yangu nitahitaji sana kusheherekea na mashabiki zangu kwa sababu wamechangia vitu vingi hadi mimi kufikia hapa, siwezi kuwaambia harusi yangu itakuwa lini ila itakapofika nitawaambia" amesema Johari.

Aidha Johari amesema kamwe hataweza kumchora mtu yeyote Tattoo, hata kama atakuwa ni mpenzi wake kwa sababu ameshindwa kufanya hivyo hata kwa wazazi wake.

"Mimi sina tattoo yoyote mwilini mwangu na sijawahi kuchora, sikumchora Baba yangu na Mama yangu ambao wamenileta duniani, halafu nichore kwa mtu niliyemkuta chini ya jua, kiukweli sijawahi kuona mtu wa kumchora".