Kauli ya BASATA baada ya Vanessa kuacha muziki

Jumatano , 24th Jun , 2020

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza, amesema uamuzi wa msanii Vanessa Mdee kuacha muziki ni mzuri kwake kwa sababu alikuwa hapati sapoti kwa mzazi wake, lakini kwa upande mwingine kukata tamaa ni mwiko au dhambi.

Msanii Vanessa Mdee upande wa kulia, Katibu Mtendaji Basata Godfrey Mngereza

Hayo ameyaeleza mapema leo Juni 24, 2020 mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wasanii wa uchoraji "tingatinga" na waandishi wa habari.

"Ni kweli kuna changamoto kwenye upande wa burudani, lakini muda mwingine kukata tamaa ni mwiko au dhambi kwa kazi ambayo unaipenda na kwa upande mwingine, inazungumzia wasanii ambao wanaishi maisha ambayo sio ya uhalisia ila na imani sio wote watakaokuwa wanaacha muziki ipo siku atarudi tu" ameeleza Godfrey Mngereza.