Ijumaa , 2nd Sep , 2016

Shindano la Dance100% linaloendeshwa na kituo cha East africa Television linaingia katika hatua ya nusu fainali kesho Jumamosi Septemba 3 , 2016 katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es salaam kuanzia saa sita kamili mchana.

Kundi la Tatanisha Crew

Akielezea maandalizi ya shindano hilo, mratibu Bhoke Egina amesema hadi sasa maadalizi yamekamilika na makundi yote yapo tayari kwa hatua ya nusu fainali baada ya kupata maelekezo kwa muda wa wiki mbili kutoka kwa majaji wa shindano.

“Mpaka sasa maandalizi yapo vyema, makundi yote yana munkari wa kuonesha ubunifu wa hali ya juu, hivyo tunawaalika watu wote kufika kutazama mambo ambayo wameandaliwa na vijana wao” amesema Bhoke.

Bhoke ameongeza kuwa katika shindano la kesho wadhamini Vodacom na Coca- Cola watatoa zawadi kwa mashabiki watakaofika kushuhudia burudani uwanjani hapo.

Makundi kumi yatashiriki hatua ya nusu fainali ambapo, matano yataaga mashindano hayo ili kupisha matano yatakayobaki kujipanga kwa ajili ya fainali.

Makundi yatakayopambana kesho kwa hatua ya nusu fainali ni J Combat Crew, Clever Boys , Mazabe Powder, Team Makorokocho, The Heroes Crew, Tatanisha Crew, Wazawa Crew , D.D.I Crew, The Quest Crew na BBK Boys.

Majaji wa Dance100%
Tags: