Alhamisi , 6th Oct , 2022

Rapa Country Wizzy amesema ametimiza miaka 10 kwenye mziki na moja ya kitu alichojifunza ni kuchukua elimu ya biashara ya mziki ambapo amekua ni mmoja wa wasanii wanaongiza pesa nyingi kupitia Digital Platform. 

Picha ya msanii Country Wizzy

"Nimekaa zaidi ya miaka 10 kwenye mziki, nimejifunza vitu vingi sana hasa kibiashara. Nimesomea miaka mitatu biashara ya mziki namna ya kuingiza pesa kwa kutumia Digital Platform".

"Nimebahatika kuwa rapa ninayeingiza pesa nyingi kila mwisho wa mwezi, ni pesa ambayo pengine wasanii wengine hawaingizi, najiona mkubwa kuuza kazi zangu na kuniingiza kipato kikubwa" ameongeza Country Wizzy