Jumatatu , 21st Oct , 2019

Msanii wa filamu Yusuph Mlela, ametoa maoni yake baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo zinasemwa mitandaoni kwamba msanii Gelly wa Rhymes, amebadilisha dini na kuwa Muislam kisa mwanamke.

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Yusuph Mlela amesema ni sawa kwa Gelly kubadilisha dini hasa kuingia katika uislam

''Ni sawa kwa sababu mimi ni muislam na yeye Gelly amekuwa muislam, namsupport na nimempokea kwa imani yangu naamini amefanya jambo sahihi na nampongeza sana kwa kufanya hivyo na uislamu ndiyo maisha" amesema Yusuph Mlela

"Ni kawaida tu halafu mapenzi yana nguvu mwisho wa siku kama kafanya kwaajili ya mapenzi ni sawa tu na si kitu kibaya kuingia katika uislam kwa hiyo hakuna shida" ameongeza 

 

Official Gelly kwa sasa anatumia jina la Ally, baada ya kuingia katika uislam na amefunga ndoa na mke wake wiki tatu zilizopita Jijini Arusha.  

Yusuph Mlela ameendeleza kusema, hata yeye yupo tayari kubadilisha dini ila isiwe tofauti na uislamu, pia tayari anamshawishi mpenzi wake Ebitoke, abadilishe dini na muda ukifika atafanya hivyo na atakuwa mke wake.