Jumapili , 31st Mar , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' amefunguka kuhusu suala la kuwa na mtoto pamoja na kufunga ndoa, ambapo amesema kuwa analifikiria bado.

Ommy Dimpoz.

Akizungumzia hilo kwenye Friday Night Live (FNL) ya EATV, Ommy amesema kuwa anatamani kuwa na familia lakini sio suala la kukurupuka kwakuwa, anahitaji kujipanga.

"Kuhusu suala la kuingia kwenye majukumu mazito, yanahitaji muda wa kujipanga sio ufanye tu kwakuwa watu wanasema hivi kuhusu wewe, acha waseme lakini maneno yao yasifanye ukurupuke", amesema Ommy.

Hivi karibuni msanii huyo alipitia kipindi kigumu cha maradhi, na kitu ambacho amekiri kuwa kimempa fundisho kubwa juu ya maisha ya binadamu kuwa si kitu hapa duniani.

Bofya link hapo chini kumtazama Ommy amefunguka zaidi.