Jumanne , 19th Mei , 2015

Baada ya kipindi kirefu cha kuona tu katika mitandao, kuhisi na pia kusikia juu ya mahusiano ya kimapenzi ya mastaa wa muziki One the Incredible pamoja na msanii Grace Matata, wameweza kuongelea kuhusu suala la malavidavi yao.

wasanii wa muziki wa bongofleva nchini One The Incredible akiwa na Grace Matata

Kwa upande wa One kuhusu mpenzi wake Grace, rapa huyo amewataka mashabiki kuendelea kufuatilia kazi zao, huku upande wa pili wa Grace akisema kuwa kwa sasa waone tu na watafahamu zaidi juu ya hilo mahusiano hayo yakichukua hatua inayofuata siku za hivi karibuni.