Jumanne , 14th Dec , 2021

Hitmaker wa wimbo wa Tetema na CEO wa Next Level Music Rayvanny anasema tangu Tanzania ipate Uhuru haijawahi kuwa na wimbo kama tetema katika ukanda wa Africa Mashariki.

Picha ya msanii Rayvanny

Kupitia page yake ya Instagram Rayvanny ameandika kwamba "Sijisifii toka tupate Uhuru haujawahi kutokea wimbo kama huu 'tetema' East Africa Period kama unabisha sema wewe upi" 

Video original ya wimbo wa tetema una views milioni 60 kwenye mtandao wa Youtube, remix ya pili ina views milioni 6 na remix ya tatu ina views milioni 10 mpaka sasa.