"Hata nikifikisha wake wanne haina maana" Jj Mwaka

Jumatatu , 15th Jun , 2020

Daktari wa tiba asilia, matatizo ya afya na uzazi kwa wanawake Dkt Mwaka, ameeleza kuwa sababu ya kuoa wake watatu ni tamaa tu, na kwamba hata mke wa pili na watatu amewaoa bila kuangalia vigezo vyovyote.

Dr Jj Mwaka akiwa na mmoja wa wake zake aitwaye Chimii

Dkt Mwaka amesema hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio, ambayo inaruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 4:00 Asubuhi - 6:00 Mchana, wakati anaeleza sababu ya kuoa wake watatu na mpango wa kuongeza mke wa nne.

"Sijawahi kuangalia vigezo vyovyote mara nyingi wanaume huwa tunaoa kwa sababu ya tamaa, unaweza ukamuona binti ukavutiwa naye kama hupendi udhinifu ndiyo unaoa, ila kiukweli kinachokusukuma hapo mwanzo ni matamanio tu, mke wangu wa pili na watatu sikutazama vigezo lakini nashukuru Mungu naishi nao vizuri mpaka leo" ameeleza.

Aidha Dkt Mwaka ameongeza kusema "Wanaume wote wanatamaa ila kinachotokea ni kujizuia tu kwa sababu mbalimbali, hata nikifikisha wake wanne haina maana kama tamaa itaisha lakini kisheria nitakuwa nimefikisha kiwango cha kutosheka nacho".