Ijumaa , 18th Jan , 2019

Klabu ya soka ya Yanga imemaliza maandalizi ya mwisho salama bila majeruhi kuelekea mchezo wake wa kesho dhidi ya Stand United ambao utachezwa saa 10:00 jioni, masaa manne kabla ya mechi ya AS Vita Club na Simba.

Wachezaji wa Yanga na Simba kwenye mazoezi.

Mchezo huo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United utapigwa kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ambao Yanga itakuwa inasaka alama 3 kwaajili ya kujikita zaidi kileleni.

''Mazoezi yetu yamekamilika salama na hakuna mchezaji yeyote mwenye majeraha kwa waliopo hapa Shinyanga wote wanaweza kutumika kazi inabaki kwa benchi la ufundi kuamua nani aanze'', amesema'', amesema daktari wa timu Dr. Bavu.

Wakati Yanga wakicheza mchezo wa kesho watakuwa wanafikisha michezo 20 ya ligi huku wapinzani wao Simba ambao saa 1:00 usiku watacheza na AS Vita Club bado wana michezo 14.

Yanga wanaongoza ligi hivi sasa wakiwa na alama 53 wakifuatiwa na Azam FC yenye alama 41 huku KMC ikiwa katika nafasi ya 3 na alama 34 na Simba wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 33.