Jumatatu , 20th Nov , 2023

Novak Djokovic ameweka rekodi ya kushinda mataji 7 ya Tenisi ndani ya kalenda ya mwaka wa mashindano wa 2023. Djkovic ameweka rekodi hiyo baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Tenisi ya Turin ATP Tour iliyofanyika Turini nchini Italia.

Novak Djokovic ameshinda mataji 7 ndani ya mwaka 2023 ikiwa ni rekodi.

Baada ya ubingwa huu Djokovic amesema huu ni msimu bora zaidi kwenye Maisha yake ya tenisi.

"Huu ni moja ya misimu bora ambao nimekuwa nao maishani mwangu bila shaka, ni maalum sana. Kushinda taji dhidi ya shujaa wa mji huu Jannik, hii wiki ni ya ajabu. Kimbinu nilicheza tofauti sana leo kuliko katika hatua ya makundi dhidi ya Jannik. Kwa ujumla, hii ni wiki ya maajabu." Alisema Djokovic

Djokovic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 36 ameweka rekodi hiyo baada ya kumfunga Jannik Sinner rai awa Italia kwa seti 2 mfululizo 6-3 na 6-3. Ubingwa huu umemfanya Djokovic afikishe mataji 7 aliyoshinda ndani ya mwaka 2023 ameshinda ubingwa wa Cincinnati Masters, Adelaide International, Paris Masters, ATP Turin na Grandslams 3 Australian Open, US Open na French Open.

Djokovic atamaliza mwaka akiwa mchezaji namba 1 kwa ubora Duniani upande wa wanaume kwenye viwango vya ubora ikiwa ni kwa mwaka wa 8 tofauti ana maliza mwaka akiwa kinara lakini leo Jumatatu anaianza wiki akiwa namba 1 ikiwa ni wiki ya 400 anaianza akiwa kama mchezaji bora Duniani kwenye msimamo.