Jumatano , 17th Jul , 2019

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, limetoa mwongozo mpya kuelekea michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL msimu ujao.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu Afrika

CAF imesema kuwa katika michezo ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho CAFCC, utapigwa mchezo mmoja pekee badala ya michezo miwili.

Pia mchezo huo mmoja utapigwa katika katika uwanja huru hauna uhusiano na timu yoyote kati ya zilizoingia fainali.

Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kuzuka kwa sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita kati ya Wydad Casablanca na Esperance de Tunis, ambao haukumalizika kwa utaratibu licha ya Wydad kutangazwa mshindi na kukabidhiwa kombe na baadaye kupokonywa.

Mwongozo huo mpya utazigusa timu wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba SC na Yanga zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika, pamoja na Azam FC na KMC ambazo zitashiriki Kombe la Shirikisho endapo zitaweza kufika hatua ya fainali.