
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia moja ya goli jana kwenye mchezo dhidi ya Newcastle
Na sasa wanongoza Ligi kwa tofauti ya alama 1 dhidi ya Manchester city walio nafasi ya pili na tofauti ya alama 4 dhidi ya Chelsea waliopo nafasi ya 3.
Mabao ya Liverpool katika ushindi huo wa kihistoria kwa klabu hiyo yamefungwa na Diogo Jota, Mo Salah ambaye alifunga bao lake la 15 msimu huu kwenye Ligi na Trent Alexander Arnold alifunga bao la tatu kwa liverpoo wakati lile la Newcatle limefungwa na Jonjo Shelvey, huu pia ulikuwa ni mchezo 32 mfululizo Liverpool wamefunga goli kwenye michuano yote.
Mpaka sasa Liverpool imeshacheza michezo 4227 kwenye Ligi England kuanzia ikiitwa Ligi draja la kwanza mpaka ilipobadilishwa na kuwa Ligi Kuu mwaka 1992, katika michezo hiyo imeshinda michezo 2000 wametoka sare 1047 wamefungwa michezo 1180 wastani wao wa ushindi ni asilimia 47.3. Mpaka sasa timu hiyo kutoka mitaa ya Merseyside imeshinda mataji 19 ya Ligi Kuu na ubingwa wa kwanza walishinda msimu wa 1900-01 na wa mwisho wameshinda msimu wa 2019-20.