
Katibu msaidizi wa JKT Ruvu Sospeter Mhabi amesema, wameangalia mahitaji ya muhimu yanayohitajika katika ushiriki wa Ligi hivyo wakaona ni vizuri wakawa na kocha Malale Hamsini ili aliyekuwa kocha wa timu hiyo Abdallah Kibaden aweze kuwa mkurugenzi wa ufundi ndani ya timu hiyo.
Mhabi amesema, pia wamefanya mabadiliko kwa upande wa wachezaji kwa kuzingatia mapungufu yaliyoonekana ndani ya kikosi hicho kwa msimu uliopita ambapo wamechukua wachezaji takribani nane kutoka vilabu vya hapa nchini.
Mhabi amewataja wachezaji hao kuwa ni Atupele Green kutoka Ndanda FC, Rahim Juma, Chuma Yusuph, Pera Ramadhan na Hassan Omary wote wakitokea African Sports ambayo imeshuka daraja, Aziz Gille kutota Mgambo JKT ambayo pia imeshuka daraja , Suma Hamis kutoka JKU, Waziri Omary kutoka Abajalo na Said Kipalo kutoka katika kituo cha kukuza vipaji vya magolikipa nchini.
Kwa upande wake Mshambuliaji wa timu hiyo Saad Kipanga amesema, anaamini msimu ujao watafanya vizuri kutokana na usajili uliofanya ikiwemo kuchukua wachezaji wakongwe ambao wataweza kusaidiana na wachezaji wapya katika ligi ii kutimiza malengo ya timu hiyo.