Morrison wa Yanga mikononi mwa Jeshi la Polisi

Alhamisi , 30th Jul , 2020

Jeshi la Polisi Dar limethibitisha kumshikilia kwa muda staa wa Yanga, Bernard Morrison katika kituo kikuu cha Osterbay, Jijini Dar es salaam.

Winga machachari wa Yanga, Berand Morrison (Pichani) akiwa mazoezini

Kamishna wa Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Kinondoni Rodgers Bukombe amesema“Morrison alikamatwa leo mchana baada ya kupishana maneno na na vijana wetu ambao walikuwa wanatilia shaka gari lake baada ya kumsimamisha kulikuwa na ukaidi fulani.

“Lakini yeye mwenyewe aliomba wampeleke polisi na kweli vijana walimchukua na baada ya kumfikisha maelezo yaliyotolewa ikaonekana kwamba ni kosa la kawaida na ambalo siyo lazima aendelee kushikiliwa kwahiyo akawa ameachiwa kwa dhamana.

“Askari anapokuwa doria anapotilia shaka kitu chochote huwa anataka ajiridhishe na uhalali juu ya kile kilichopo kwenye eneo hilo, walitaka kujua kwenye gari yake kuna nini kukatokea mabishano,” alisema kamanda huyo wa Jeshi la Polisi.

Nyota huyo raia wa Ghana yupo katika mgogoro na klabu ya Yanga unaohusisha masuala ya mkataba na hadi msimu unamalizika hakushiriki katika maadhi ya michezo na klabu yake.