Mtibwa Sugar iliyokuwa inashika nafasi ya tano kabla ya kushinda mchezo wa raundi ya 13 dhidi ya Lipuli FC, sasa imepanda hadi nafasi ya tatu ikizizidi klabu za Yanga SC iliyokuwa nafasi ya nne pamoja na Singida United iliyouwa nafasi ya tatu.
Mtibwa Sugar imefikisha pointi 24 katika mechi 13, na kuizidi Singida yenye pointi 21 pamoja na Yanga yenye pointi 21 hivyo kufanya timu hizo ziwe na kazi ngumu ya kushinda mechi zao za raundi ya 13 ili kuipindua timu hiyo.
Singida United watashuka dimbani alhamisi ijayo kucheza na vinara wa ligi Simba SC huku mabingwa wapya wa Kombe la mapinduzi Azam FC pia watacheza mechi yao ya raundi ya 13 siku hiyo.
Mabingwa watetezi Yanga SC watacheza na timu ya Mwadui FC Januari 15, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


