
Mwanadada huyo wa kijerumani Angelique Kerber amemshaza mchezaji namba moja duniani Serena Williams katika seti tatu za 2-6 6-4 7-5 na kushinda taji lake la kwanza kubwa la Grand Slam la michuano ya wazi ya Australia.
Kerber, mchezaji namba saba duniani mwenye miaka 28 kwa ushindi wa mchezo huo uliopigwa katika jiji la Melbourne Park anakuwa mjerumani wa kwanza kushinda taji kubwa kwa mchezaji mmoja mmoja tangu lipofanywa hivyo na mchezaji Steffi Graf mwaka 1999 katika michuano ya wazi ya Ufaransa.
Kipigo hicho kwa Serena Williams, mwenye miaka 34, ni cha tano katika fainali 26 za michuano mikubwa ya Grand Slam na kupoteza nafasi ya kuweka rekodi yakutwaa mataji 22.
Katika hatua nyingine, Jamie Murray amekuwa mchezaji wa tenis wa kwanza kutoka Visiwa vya Uingereza kushinda michuano ya wazi ya Australia kwa upande wa wanaume katika kipindi cha miaka 82 kwa wachezaji wawili wawili.
Rekodi hiyo inatokana na ushindi alioupata leo akishirikiana na Bruno kuwafunga Daniel Nestor na Radek Stepanek kwa seti 2-6 6-4 7-5.
