Sevilla yathibitisha kushirikana na Yanga

Ijumaa , 19th Jun , 2020

Klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kupitia tovuti ya klabu hiyo imethibitisha kuingia mkataba wa miaka mitatu na nusu kuwa washauri wa klabu ya Yanga ya Tanzania. 

Klabu ya Yanga na Sevilla

La Liga na Sevilla FC kwa pamoja  zimesaini mkataba wa makubaliano ya kimkakati ya kuwa washauri wa Yanga na kuhakikisha Yanga  inafanikiwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza soka la Afrika.

Wasimaizi hao wa soka la Hispania wataishauri klabu ya Yanga zaidi katika maeneo ya muundo wa utawala, uchumi na usimamizi wa mashabiki.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa wa La Liga, Oscar Mayo amesema ni makubaliano ya miaka mitatu na nusu ambayo watawashauri katika muundo wa utawala, masoko na mauzo, mabadiliko ya kidigitali, udhibiti wa uchumi, maendeleo ya kimataifa na usimaiszi wa mahabiki.