Ijumaa , 20th Jan , 2023

Mwenyekiti wa klabu ya Simba anayemaliza muda wake, Murtaza Mangungu amejinasibu kuwa, katika kipindi chake cha miaka miwili ya Uongozi Simba imeongeza mapato na kufikia bilioni 13 kutokana na usimamizi makini katika rasilimali za timu hiyo.

Mangungu ambaye pia anagombea kutetea nafasi yake ya mwenyekiti, amesema endapo atapewa dhamana ya kuendelea kuiongoza Simba SC basi atasimamia malengo makuu ya klabu na kila moja na hata ikitokea atakosa basi ataendelea kusalia kuwa Mwanasimba.

"Mipango ya Bodi ni kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika, tunataka kujenga miundo mbinu. nimekuwa tayari na nipo tayari kushirikiana na Mwanasimba yoyote kwa ajili ya maendeleo ya Simba. Naombeni kura zenu.

"Mapato ya klabu yameongezeka wakati naingia tulikuwa tunakusanya bilioni nne kwa mwaka lakini sasahivi tunaingiza bilioni 13. Wengi wanaonipinga ni maslahi binafsi yao binafsi," amesema Mangungu

Mwenyekiti Mangungu ambaye Ijumaa ya leo Januari 20, 2023 amezindua kampeni yake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa timu hiyo unaotaraji ufanuka Januari 29 mwaka huu, pia ametumia nafasi hiyo