Jumatatu , 19th Mei , 2014

Bonanza la michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoa wa Dar es salaam, limekusanya mamia ya wanafunzi toka shule mbalimbali, na wamepata mafunzo ya mchezo wa cricket toka kwa wakufunzi wa mchezo huo, kutoka chama cha cricket Tanzania (TCA).

Chama cha mchezo wa cricket Tanzania TCA kimeendelea na mpango wake wa kukuza mchezo huo hapa nchini baada ya hii leo kuendesha bonanza la mafunzo maalumu ya mchezo huo lililofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya mlimani likishirikisha shule mbalimbali za msingi zaidi ya 20 toka jijini dare s salaam

Mratibu wa bonanza hilo ambaye pia ni mkufunzi wa cricket toka TCA Hamis Abdalah amesema lengo ni kuhakikisha wanakuza mchezo huo kwa kuwafundisha vijana hasa wa shule za msingi kwani chimbuko la wanamichezo bora katika michezo mbalimbali duniani kote huanzia mashuleni.