Jumatano , 16th Mar , 2016

Waamuzi watakaosimamia mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Klabu ya Yanga dhidi ya APR utakaopigwa Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wanatarajiwa kuwasili hapo kesho Usiku.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema, waamuzi watakaosimamia mchezo huo watatokea visiwa vya Shelisheli huku kamishna wa mchezo akitokea nchini Afrika kusini.

Muro amesema, katika mchezo huo wao kama timu wenyeji kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka nchini TFF wameamua kuweka viingilio ambavyo vitakuwa rafiki kwa mashabiki na kuwafanya mashabiki kufika kwa wingi Uwanjani kwa ajili ya kuipa Sapoti Klabu ya Yanga