Alhamisi , 8th Jun , 2017

Kevin Durant aliweka mrusho wa pointi 3 (three-pointer), zikiwa zimebaki sekunde 45.3, na kufunga jumla ya pointi 31, wakati Golden State Warriors wakiichapa Cleveland Cavaliers 118-113 usiku wa kuamkia leo, na kuongoza 3-0 hadi sasa.

Kelvin Durant kulia pamoja na Stephen Curry

Hakuna timu iliyowahi kufungwa 3-0 na kupindua matokeo ya ushindi, na kama Warriors watashinda mchezo wa nne Ijumaa, watakuwa wametawazwa ubingwa wa NBA kwa mwaka 2017, na hivyo kuwanyan'ganya Cavaliers kombe hilo walilotwaa msimu uliopita.

Timu nane pekee ziliwahi kuwaondosha wapinzani wao 4-0, huku mechi ya mwisho ilikuwa pale San Antonio Spurs ilipowaondosha Cleveland Cavaliers msimu wa mwaka 2006-07.

Warriors imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda michezo 15 mfululizo ya kumaliza msimu, kutoka kwenye ligi kubwa nne za michezo nchini Marekani, ambazo ni NFL, NBA, MLB na NHL.