
Wachezai wa kikosi cha Singida Big Stars
Septemba 2,2022 kikosi cha Singida United kinatarajiwa kuelekea nchini Rwanda ambapo wamealikwa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports.
Ofisa Habari wa Singida Big Stars Hussein Massanza amesema kuwa wachezaji wote wataondoka kuelekea nchini Rwanda.
“Tutaondoka na wachezaji wote ambao tumewasajili kwa ajili ya mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports utakaochezwa Uwanja wa Nyamirambo.
“Msafara huo utajumuisha benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi na mchezo wetu unatarajiwa kuchezwa Septemba 4 huku gharama zote zitagharamiwa na wenyeji wetu,” amesema Massanza.
Miongoni mwa nyota wa kikosi hicho watakaoibukia Rwanda ni pamoja na Pascal Wawa, Deus Kaseke, Metacha Mnata.