East Afrika Redio imeshuhudia chupa zilizojaa haja ndogo (Mikojo) katika eneo la kijiwe cha Madereva hao hali inayotishia afya za Madereva na watumiaji wengine wa magari yao.
Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa umoja wa Madereva wa magari ya Mizigo,eneo la mwanjelwa EPHRAHIM JUMA amesema kukosekana kwa choo katika eneo hilo imekuwa ni kero yao ya Muda Mrefu.
IPYANA NJIRO na ALIKO JUMA ambao ni Madereva wa Mwanjelwa wameeleza kukerwa na hali hiyo huku wakiiomba mamlaka husika kuchua hatua za haraka ili kuwaondolea changamoto hiyo.