Ijumaa , 23rd Nov , 2018

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema wamefikia maadhimio ya kubadilishana taarifa za kiuharifu pamoja na waharifu wenyewe na nchi wanachama wa Polisi wa kimataifa (INTERPOL).

Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro.

Sirrro ameyasema hayo baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai ambako alihudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa INTERPOL ulioshirikisha nchi wanachama 195.

Sirro ameweka wazi kuwa katika mkutano huo imebainika kuwa kuna mapungufu makubwa ya kubadilishana taarifa za uharibu ama waharifu baina ya nchi wanachama pamoja na uchunguzi wa makosa ya kimtandao hivyo kwa pamoja wamekubaliana kuanza kubadilishana pale inapohitajika.

''Tumejadili namna bora ya kubadilishaba taarifa za waharifu na waharifu pale wanapokuwa wamekamatwa lakini pia kuanzisha kikosi maalum cha vijana wenye utaalam wa makosa ya mtandao ili kusaidia kutoa elimu juu ya makosa ya mtandao'', amesema Sirro.

Aidha Sirro ameeleza kuwa mkutano huo pia umejadili namna ya kukabiliana na ugaidi ambao kwasasa upo dunia nzima hivyo wamekubaliana kila nchi kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukabiliana na hilo.