Jumatatu , 21st Jun , 2021

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla, amewataka wakuu wa wilaya wapya kwenda kushirikiana na viongozi wengine watakaokutana nao katika maeneo yao ya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla

RC Makalla ametoa rai hiyo leo baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya wapya ndani ya mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Anatoglo.

 Mhe.Fatma Nyangasa akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

“Nendeni mkashirikiane na mtakao wakuta mmoja ya mambo tunalokoseaga sana pale unapohamia unaanza kusikiliza watu, ukifika unaanza kuona kila mtu adui nendeni mkafanye kazi na wote mtakao wakuta katika eneo husika,” amesema RC Makalla.

 Mhe. Kherry James akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

“Sisi tulifika tukaanza kazi hatujataka kujua hapa kuna nani na nani, tunachojali ni nafasi zao na ushauri wao kule mtakapoenda mtamkuta mtandao wa uongozi mzima umekamilika usianze na lako jipya toa ushirikiano mfanyekazi,” amesema RC Makalla.

Aidha, RC Makalla amesisitiza mambo matano ambayo ni kukusanya mapato, kutatua kero za wananchi, kusimamia ulinzi na usalama, kusimamia usafi pamoja usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Wakuu wa Wilaya wapya walioapishwa leo ni DC wa Kigamboni Fatma Nyangasa na DC wa Ubungo Kherry James.